Everton imefanikiwa kuondoka na
pointi moja muhimu katika dimba la Etihad, baada ya wenyeji
Manchester City kulazimisha sare ya goli 1-1.
Katika mchezo huo ambao wenyeji
Manchester City walikuwa wameutawala kwa asilimia kubwa walijikuta
wakimaliza kipindi cha kwanza bila kuliona goli la Everton.
Kipa wa Everton Martin Stekelenburg
alikuwa shujaa baada ya kupangua penati mbili ya kwanza ikipigwa na
Kevin De Bruyne na ya pili iliyopigwa na Sergio Aguero.
Everton alikuwa ya kwanza kufunga
goli latika kipindi cha pili kupitia kwa Romelu Lukaku, lakini
Manchester City ilipambana kiume na kusawazisha kupitia kwa Nolito.
Kipa Martin Stekelenburg akipangua penati ya Kevin De Bruyne
Romelu Lukaku akiachia shuti lililojaa wavuni na kuandika goli la kwanza kufungwa katika mchezo huo
Mpira wa kichwa uliopigwa na Nolito ukimshinda kipa wa Everton na kuandika goli la kusawazisha la Manchester City
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni