Mwanamuziki nyota wa Marekani, Chris
Brown, amempora simu shabiki wake mmoja mwanamke nchini Kenya
aliyekuwa akitaka kupiga naye picha ya Selfie na kisha kuipigiza
chini kwa hasira.
Tukio hilo limetokea katika uwanja
wa ndege wa Kimataifa wa Moi, wakati msanii huyo anayejulikana kwa
ukorofi Chris Brown alipotua Mombasa kwa ajili ya shoo aliyoifanya
mwishoni mwa wiki.
Mwanamke huyo Brenda Chepkoech
alijikuta simu yake aina ya I-Phone 6 ikiporwa na Brown bara baada ya
kumsogelea na kuanza kupiga naye Selfie na kisha kuipigiza chini
baada ya kuingia kwenye gari.
Brenda Chepkoech akiwa ameshikilia simu yake ya I-Phone 6 ambayo iliharibika kioo baada ya kupigizwa chini na Chris Brown
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni