Mshambuliaji wa Ubelgiji, Christian
Benteke, amefunga goli la mapema mno kuwahi kufunga katika hatua ya
kuwania kufuzu kuntinga michuono ya kombe la dunia baada ya kufunga
katika sekunde ya saba dhidi ya Gibraltar.
Mshambuliaji huyo wa timu ya Crystal
Palace pia katika mchezo huo amefanikiwa kutikisa nyavu mara tatu
yaani hat-trick wakati Ubelgiji ikishinda kwa ushindi mnono wa magoli
6-0 katika mchezo wa kundi H.
Kwa goli hilo la Benteke limeipita
rekodi ya goli lililoweka rekodi ya kufungwa mapema katika michuano
hiyo lililofungwa sekunde ya 8.3 na Davide Gualtieri wa San Marino
dhidi ya Uingereza mwaka 1993.
Axel Wisel akishangilia goli la pili alilofunga kwa shuti la mita 25
Katika mchezo mwingine wa kuwania
kufuzu kutinga michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 kiungo wa
Manchester United, Paul Pogba ameifungia Ufaransa goli la shuti la
mbali na kuisaidia kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Uholanzi.
Mpira uliopigwa na Paul Pogba ukitinga wavuni huku kipa wa Uholanzi akiwa ameanguka chini asijue la kufanya
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni