Cristiano Ronaldo amepata msaidizi
katika ufungaji, wakati Ureno ikiichakaza Faroe Islands kwa magoli
6-0 katika mchezo wa kuwania kufuzu kutinga michuano ya kombe la
dunia.
Kinda Andre Silva, 20, anayechezea
Porto alifunga magoli matatu yaani hat-trick katika kipindi cha
kwanza na kisha Ronaldo kuongeza la nne katika kipindi cha pili.
Katika dakika za mwisho Joao
Moutinho aliongeza la tano huku Joao Cancelo akikamilisha goli la
sita kwa Ureno.
Kinda Andre Silva akipachika goli la kwanza la Ureno
Cristiano Ronaldo akidhibitiwa na kuanguka chini
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni