.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 11 Oktoba 2016

WALIMU KUHAMASISHA MASOMO YA SAYANSI

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akikabidhi Tuzo ya Mwalimu Bora
kwa Mwalimu Pili Omari Makota wa shule ya Msingi Uraki katikati ni
Mkurugenzi wa Shirika la The Foundation For Tomorrow Melissa Queyquep. Tuzo za Walimu Bora ziliandaliwa na shirika lisilokua la kiserikali la The
Foundation For Tomorrow jana jijini Arusha na kufanyika katika shule ya
msingi Arusha schoo
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akikabidhi Tuzo ya Mwalimu Bora
kwa Mwalimu Regina Lekule wa shule ya Msingi Msitu wa Mbogo, katikati ni
Mkurugenzi wa Shirika la The Foundation For Tomorrow Melissa Queyquep. 


Tuzo za Walimu Bora ziliandaliwa na shirika lisilokua la kiserikali la The
Foundation For Tomorrow jana jijini Arusha na kufanyika katika shule ya
msingi Arusha school

                                                                                           Na Woinde Shizza,Arusha

Walimu nchini wametakiwa kuhamasisha Wanafunzi kusoma masomo ya Sayansi hasa katika kipindi hiki ambacho taifa linaelekea kwenye uchumi wa viwanda ili kuweza kupata wataalamu wa kutosha.

Akizungumza katika Utoaji wa Tuzo kwa walimu bora katika wilaya ya Arusha
mjini na Arumeru ,Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro amewataka
Walimu nchini kuwa wabunifu na kuwahamasisha wanafunzi kupenda masomo ya sayansi ambayo ni chachu ya maendeleo ya nchi.

Alisema kuwa serikali inatambua kuwa Walimu ni Injini ya elimu bila walimu
elimu haiwezi kusonga mbele hivyo walimu watumie nafasi zao katika
kuhakikisha kuwa serikali inavuna wataalamu waliobobea katika masomo ya
sayansi kwa kuwajengea misingi bora.

“Hatuwezi kupata Wataalamu wa kutosha viwandani kama hatutahamasisha masomo ya sayansi mashuleni nchi itakuwa na utegemezi mkubwa wataalamu kutoka nje ya nchi” Alisema Mkuu wa Wilaya

Mkurugenzi wa Shirika la The Foundation For Tomorrow Melissa Queyquep ambao ni waandaaji wa tuzo hizo alisema kuwa Tuzo hizo zimetolewa kwa walimu kwa kutambua mchango wa Walimu katika kuhakikisha kuwa Watoto wanapata elimu bora itakayowakomboa kifikra,kijamii na kiuchumi.

“Tumezingatia vigezo vingi katika utoaji wa tuzo hizi ikiwemo uwezo wa
kuchochea ufikiri na uchambuzi kwa watoto,Ubunifu na uvumbuzi,Anafundisha kwa mifano zaidi kuliko maelezo,uwezo wa kushawishi na kuhamasisha wanafunzi kujifunza,haiba pamoja na uzoefu kazini” Alisema Melisa

Jumla ya Walimu 10 wamepata tuzo za Walimu bora kutoka Wilaya ya Arusha
mjini na Wilaya ya Arumeru,Baadhi ya Walimu hao ni Regina Lekule,Ally
Msongo,Pili Mokoka,Evelina Sanga,Neema Lema,Swahibu Issa,Nicholous
Michael,Frida Malia,Asumpta Mbuda na Paulina Lolo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni