Cristiano Ronaldo amecharuka na
kufunga magoli manne kwa timu yake ya taifa ya Ureno wakati
ikiiangushia kipigo kizito Andorra cha magoli 6-0 katika mchezo wa
kuwania kufuzu kutinga kombe la dunia mwaka 2018.
Cristiano Ronaldo alifunga mara
mbili kwa kichwa katika dakika nne za kwanza za mchezo
huo na kuwafanya mabingwa hao wa Euro 2016 kutawala mchezo huo.
Joao Cancelo aliifungia Ureno goli
la tatu na kisha baadaye Ronaldo kufunga la nne katika dakika ya 42
na kufikisha hat trick yake ya 42 katika rekodi yake ya uchezaji
soka.
Ronaldo alifumania nyavu tena na pia
Andre Silva akafunga goli la sita katika mchezo huo ulioshuhudia
wachezaji wawili wa Andorra wakitolewa nje kwa kadi nyekundu.
Cristiano Ronaldo akifunga goli la kwanza kwa mpira wa kichwa
Cristiano Ronaldo akifunga goli lingine kwa mpira wa kichwa
Cristiano Ronaldo akifunga goli la tatu kwa shuti alilopiga kitaalam




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni