Eden Hazard, Romelu Lukaku na Toby
Alderweireld wameifungia Ubelgiji na kuisaidia kuibuka na ushindi wa
magoli 4-0 dhidi ya Bosnia, katika mchezo wa kuwania kufuzu kutinga
fainali za kombe la dunia 2018.
Katika mchezo huo Ubelgiji walipata
goli la kwanza kufuatia goli la kujifunga la Emir Spahic, ambaye
alijikuta akitumbukiza mpira wavuni katika harakati za kuuokoa.
Eden Hazard aliongeza goli la pili
baada ya kumzungusha kipa Asmir Begovic na kisha Toby Alderweireld
akaongeza la tatu kwa mpira wa kisigino na Lukaku akakamilisha goli
la nne.
Eden Hazard akimpiga chenga kipa Begovic na kufunga goli
Romelu Lukaku akiachia shuti lililojaa wavuni na kuandika goli la nne



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni