.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 8 Oktoba 2016

KEVIN GAMERO AFUNGA MAWILI WAKATI UFARANSA IKIIBUKA NA USHINDI DHIDI YA BULGARIA

Timu ya taifa ya Ufaransa imeanza vyema mchezo wake wa kwanza wa kuwania kufuzu kutinga michuano ya kombe la dunia 2018, kwa kupata ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Bulgaria.

Katika mchezo huo wenyeji Ufaransa ilijikuta ikifungwa goli katika dakika ya sita kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Mihail Aleksandrov, lakini Kevin Gamero akasawazisha kwa kichwa cha kuchupa.

Mchezaji wa West Ham, Dimitri Payet aliipatia Ufaransa goli la pili, huku Antoine Griezmann akiongeza goli la tatu alilolifunga kwa utulivu na kisha Gameiro akifunga tena goli la nne.
                  Kevin Gamero akifunga goli la kusawazisha kwa mpira wa kichwa cha kuchupa
                                         Antonio Griezmann akifunga goli la tatu la timu ya taifa ya Ufaransa 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni