Askofu Dedmond Tutu wa Afrika Kusini
amebainisha kuwa anataka kuwa na fursa ya kuomba kusaidiwa kufa.
Mshindi huyo wa tuzo ya Nobel na
mwanaharakati wa kupinga ubaguzi, amesema hataki kulazimishwa
kuendelea kuishi kwa gharama zozote.
Matamshi hayo ya Tutu yameandikwa na
yeye katika gazeti la Washghton Post wakati akitimiza miaka 85 ya
kuzaliwa.
Mnamo mwaka 2014 Askofu Tutu
alibainisha kuwa anaunga mkono wagonjwa mahututi kusaidiwa kufa,
lakini alikuwa hajaeleza iwapo yeye pia angependa kusaidiwa kufa.
Mwezi uliopita Askofu Tutu alikuwa
amelazwa na kufanyiwa upasuaji ili kumtibu maambukizi ambayo yamekuwa
yakijirudia rudia.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni