Dereva Lewis Hamilton amepunguza
pointi za ubingwa dhidi ya Nico Rosberg wakati wakipata ushindi kwa
urahisi katika mbio za Grand Prix za Marekani.
Ushindi huo wa Hamilton ni wa kwanza
tangu ashinde mbio Grand Prix za Ujerumani mwezi Julai na kumuweka
pointi 26 nyuma ya dereva mwenzake wa Mercedes huku pointi 75 zikiwa
zimebakiwa katika mbio tatu.
Rosberg alimaliza wa pili baada ya
kufanikiwa kuitwa nafasi hiyo iliyopotezwa na timu ya Red Bull na
dereva Daniel Ricciardo. Muaustralia huyo alimalizia wa tatu mbele ya
dereva wa Ferrari, Sebastian Vettel.
Lewis Hamilton akiwa amesimama juu ya gari lake baada ya kushinda


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni