Diego Costa na Nolito wamefunga goli
kila mmoja katika kipindi cha pili na kuifanya Hispania kushinda kwa
magoli 2-0 dhidi ya Albania hapo jana na kuongoza kundi G katika
kuwania kufuzu kutinga michuano ya kombe la dunia 2018.
Mshambuliaji huyo wa Chelsea
alitumia vyema kosa la kizembe la Albania, Etrit Berisha katika
dakika ya 56 katika mchezo uliokuwa ukichezwa huku mvua ikinyesha
huko Shkoder na kisha baadaye Nolito kufunga la pili akitokea benchi.
Diego Costa akijaribu kukatiza kati kati ya mabeki wa Albania
David Silva hakuwa mchoyo baada ya kutoa pande hili kwa Diego Costa na kufunga
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni