Timu ya taifa ya Wales imekumbana na
kigingi katika kampeni zake za kuwania kufuzu kutinga michuano ya
kombe la dunia mwaka 2018, baada ya kutoa sare ya 1-1 na timu ndogo
ya Georgia.
Katika mchezo huo alikuwa Gareth
Bale aliyeipatia Wales goli kwa mpira wa kichwa lakini Georgia,
iliyonafasi ya 137 kisoka duniani ilisawazisha kupitia kwa Tornike
Okriashvili.
Mchezaji nyota wa Wales na Real Madrid, Gareth Bale, akiwa juu baada ya kuupiga kichwa mpira uliozaa goli
Mchezaji Tornike
Okriashvili akisawazisha goli la kichwa baada ya mabeki wa Wales kuzembea kumkaba
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni