Kapteni wa Barcelona, Andres
Iniesta, atakuwa nje ya uwanja kwa wiki sita baada ya kuumia goti
katika mchezo ambao waliibuka na ushindi wa dakika za mwisho dhidi ya
Valencia.
Kiungo huyo wa Barcelona aliumia
baada ya kukabwa na Enzo Perez baada ya dakika 14 za mchezo
walioshinda kwa magoli 3-2 na kutolewa nje kwa machela.
Iniesta atakosa michezo yote ya Ligi
ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi, na ni dhahiri sasa hatoshuka
dimbani kuivaa Manchester City Novemba mosi.
Andres Iniesta akiwa chini akipiga kelele kwa maumivu baada ya kuumia goti
Iniesta akiwa amewekwa kwenye machela ili kusaidiwa kutoka uwanjani baada ya kuumia goti



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni