Timu za Liverpool na Manchester
United zimetoka sare tasa katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza,
ambao ulikuwa unafuatiliwa mno na wapenzi wa soko duniani kutokana na
ushindani mkubwa ulipo baina ya timu hizo.
Katika mchezo huo shujaa alikuwa
kipa wa Manchester United David de Gea, ambaye aliruka na kupangua
mipira iliyopigwa na Emre Can pamoja na Philippe Coutinho kutokea
umbali wa yadi 25.
Kikosi cha Jurgen Klopp kilihitaji
ushindi ili kiwe na pointi sawa na vinara Manchester City, lakini
kikosi cha Jose Mourinho kilicheza kwa kujilinda na kilionyesha
nidhamu ya hali ya juu ya umakini.
Emre Can akipiga mpira uliopanguliwa kiufundi na kipa David de Gea
Kipa David de Gea akiruka kiufundi kupangua mpira uliopigwa na Can
David de Gea tena akiokoa mpira uliopigwa na Philippe Coutinho
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni