Watu wapatao 20 wamekufa katika
tukio la moto uliotokea kwenye hospitali Mashariki mwa India.
Polisi wamesema moto huo umetokea
katika chumba cha wagonjwa mahututi kwenye hospitali ya binafsi ya
SUM, mjini Bhubaneswar katika jimbo la Orissa.
Makumi ya wagonjwa wamepelekwa
katika hospitali zingine katika mji huo.
Askari wa zimamoto 120 wameitwa
kukabiliana na moto huo, ambao baadaye ulifanikiwa kuzimwa. Waziri
Mkuu Narendra Modi ameshtushwa na tukio la moto huo.
Vikosi vya zimamoto vikipambana kuzima moto huo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni