.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 28 Oktoba 2016

KUMBUKUMBU YA BABA YETU OMUTWALE PASCHAL RUTAIHWA KAKIZIBA

                                                          OMUTWALE Paschal Rutaihwa Kakiziba
 

                                                             13 JULAI 1935 – 28 OKTOBA 2004

Baba yetu mpendwa umetimiza mwaka wa 12 tangu ulipotwaliwa na Bwana. Picha yako inatukumbusha uwepo wako tulipokuwa sote hapa duniani, na hasa ukarimu, upendo, upole, uchangamfu na wingi wa busara.
 

Ni vigumu kukubali kwamba haupo nasi lakini hatuna budi kuamini kwamba uko nasi kiroho kwa vile tunaye Mungu ambaye anaendelea kututia nguvu kila iitwapo leo. Busara zako na ucheshi wako vinazidi kutuimarisha kila siku na tunaendelea kuzingatia maneno yako uliyokuwa ukihimiza juu ya kuwa na upendo na umoja katika familia huku tukiendelea kumtumaini Mungu wetu ambaye amekuita kwake.

Mke wako Mary-Hilda Kakiziba, rafiki yako Galita, watoto wako, wajukuu, wakwe zako, dada zako, kaka zako na wadogo zako, ndugu, marafiki na majirani wanakosa ucheshi na ushauri wako na wanakukumbuka daima.

MISA YA KUMBUKUMBU ITAFANYIKA JUMAPILI, OKTOBA 30, 2016, SAA 3 ASUBUHI KWENYE KIGANGO CHA MT. ANTHONY WA PADUA, BOKO, DSM.

Tumaini letu linajengwa na neno lisemalo: ”Umevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo umeumaliza na imani umeilinda” (2Tim. 4:7)

Tunakuomba Ee Bwana uendelee kuipumzisha roho yake mahali pema peponi, AMEN.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni