.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 28 Oktoba 2016

WATATU NJE CITY VS MAJIMAJI KESHO

WAKATI kikosi cha mbeya City fc kikitarajiwa kushuka ndimbani hapo kesho kucheza mchezo namba 98 wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya Majimaji fc ya Songea kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa,taarifa imetolewa kuwa nyota watatu kikosini wataukosa mchezo huo.

Muda mfupi uliopita Ofisa habari wa City, Dismas Ten,ameidokeza mbeyacityfc.com kuwa nyota watatu Ayoub Semtawa,John Kabanda na Omary Ramadhani hawatakuwa sehemu ya mchezo wa kesho hii ni kwa sababu ya kupisha majeraha waliyopata kwenye michezo mitatu ambayo City imecheza ikiwa nje ya uwanja wa nyumbani(Sokoine).

“Nimezungumza na daktari wetu leo asubuhi, amenifahamisha kuwa hakuna uwezekano wa kuwatumia wachezaji Ayoub Semtawa, Omary Ramadhani na John kabanda kwa sababu bado hawajapona majeraha yao waliyoyapata kwenye michezo yetu iliyopita,kulikuwa na dalili na kupona kwa Omary lakini taarifa ya mwisho ndiyo hiyo kuwa hakuna uwezekano huo kwa sasa,” alisema.

Akiendelea zaidi, Ten alisema kuwa, Ayoub semtawa aliyeumia kwenye mchezo dhidi ya African Lyon atalazimika kukaa nje kwa wiki tatu zaidi kabla ya kurejea uwanjani huku Kabanda na Omary wanaweza kuwa tayari kwa ajili ya mchezo wa tarahe mbili dhidi ya Young Africans.

“Tunaweza kuwatumia Omary na Kabanda kwenye mchezo ujao lakini hakuna uwezekano wa Semtawa kurejea uwanjani kwa sasa, daktari amesema atalazimika kukaa nje kwa majuma matatu zaidi hii ni kwa sababu alichanika nyama za paja ambazo zinahitaji muda kidogo wa mapumziko kabla ya kurejea”.

Katika hatua nyingine Ten aliweka wazi kuwa walinzi, Hassan Mwasapile na Haruna Shamte waliokuwa nje kwa majeraha tayari wamerejea kikosini na wamekuwa sehemu ya kikosi kwenye mazoezi ya siku tano yaliyofanika kwenye uwanja wa Sokoine kujiandaa na mchezo wa kesho hivyo hakuna shaka yoyote kuwa wanakuja kuimarisha safu ya ulinzi ya City.

“Taarifa nzuri kikosini ni kuwa Hassani Mwasapile na Haruna Shamte wanarejea kikosini, hili ni jambo jema kwa saababu wanakuja kuimarisha safu yetu ya ulinzi katika kuhakikisha tunaibuka na ushindi, uwepo wao utampa nafasi nzuri kocha wetu Kinnah Phiri kupanga kikosi ambacho kitampa matokeo”, alimaliza.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni