Mchezaji nyota duniani Lionel Messi
amefunga magoli matatu 'hat-trick' wakati Barcelona ikiiadhibu
Manchester City iliyobakia na wachezaji 10 dimbani kwa magoli 4-0
katika mchezo wa Ligi ya mabingwa Ulaya.
Kocha wa Manchester City, Pep
Guardiola alirejea Nou Camp na kuonyesha kumiliki mpira vizuri katika
kipindi cha kwanza lakini baadaye wakafanya makosa mengi,
yaliyopelekea kupata kipigo hicho.
Messi alipata goli la kwanza baada
ya Fernandinho kuteleza na kisha baadaye Kevin de Bruyne akapoteza
mpira na kumpa fursa Andres Iniesta kutoa pande kwa Messi akitumia
mguu wake wa kushoto kufunga la pili.
Kipa wa Manchester City alitolewa
nje kwa kudaka mpira nje ya boksi dakika chache baadaye Messi tena
akaongeza la tatu. Bacelona nao walijikuta wakibakia 10, baada ya
Jeremy Mathieu kupewa kadi ya pili ya njano dakika 15 kabla ya mpira
kuisha.
Lionel Messi akipiga mpira uliozaa goli la kwanza la Barcelona
Kocha Pep Guardiola akishikilia kichwa kusikilizia maumivu ya kipigo alichopata kutoka kwa timu yake ya zamani ya Barcelona
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni