Liverpool imepata ushindi wa 2-1
dhidi ya West Brom, lakini wakaruhusu kufungwa goli la dakika za
mwisho na kuwanyima nafasi ya kuongoza msimamo wa Ligi Kuu ya
Uingereza.
Kikosi hicho cha Jurgen Klopp
kiliutawala mchezo huo katika dimba la Anfield na kupata goli la
kwanza kupitia kwa Sadio Mane aliyeunganisha krosi ya Roberto
Firmino.
Philippe Coutinho alifunga goli la
pili akiunasa mpira uliopigwa na Mane, hata hivyo beki Gareth McAuley
alichomoa goli moja baada ya Liverpool kushindwa kuokoa mpira wa
kona.
Sadio Mane akipiga mpira na kufunga goli la kwanza la Liverpool
Philippe Coutinho akipiga mpira uliomshinda kipa Ben Foster na kuandika goli la pili



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni