Maelfu ya waombolezaji nchini
Thailand wamejipanga kwenye Mitaa ya Bangkok, wakati mwili wa Mfalme
wao Bhumibol Adulyadej ukitolewa hospitali na kupelekwa kwenye jumba
la mfalme.
Mfalme huyo aliyekaa madarakani kwa
muda mrefu kuliko wote duniani alifariki dunia jana Alhamis akiwa na
miaka 88 baada ya kuugua, na kulifanya taifa hilo kuingia kwenye
maombolezo.
Serikali ya Thailand imetangaza
maombolezo rasmi ya mwaka mzima. Mwana wa mfalme huyo Maha Vajiralongkorn ametajwa kuwa ni
mrithi wake, lakini ameomba kucheleweshwa kwa mchakato wake.
Waombolezaji wakiwa wamejipanga kungojea kuona mwili wa mfalme wao
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni