Shirikisho Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linaalika umma kuwania zabuni ya kubuni mwonekano mpya wa jezi mpya za timu ya taifa zitakazotumika kwa msimu wa 2017/18 na msimu wa 2018/19.
Kwa taarifa hii, TFF imefungua milango kwa umma ambako mtu mmoja mmoja anaweza kuwasilisha ubunifu wa mwonekano wa jezi hizo katika ofisi zake zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume ulioko kwenye makutano ya barabara za Uhuru na Shaurimoyo, Ilala jijini Dar es Salaam.
Wakati mwisho wa kupokea zabuni hizo ni Novemba 30, 2016, sharti kwa mbunifu ni kutoiga ubunifu kutoka makampuni makubwa ya vifaa vya michezo. Na Mbunifu Bora au Mshindi wa jezi ambazo zitakuwa lazima ziwe na nembo ya TFF na Bendera ya Taifa, atazawadiwa shilingi milioni mbili (Sh milioni 2).
Jezi za sasa za Timu ya Taifa ni rangi ya bluu kwa michezo nyumbani na nyeupe mechi za ugenini.
LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA OKTOBA 15 NA 16
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea leo Jumamosi Oktoba 15, 2016 kwa michezo mitatu ambako Simba inayoongoza katika msimamo wa kuwania taji hilo katika timu 16 itaikaribisha Kagera Sugar ya Kagera kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo Na.73, mwamuzi atakuwa Hussein Athuman kutoka mkoani Katavi ambako pembeni atasaidiwa na Joseph Bulali wa Tanga na Silvester Mwanga wa mkoani Kilimanjaro wakati Soud Lila wa Dar es Salaam atakuwa mwamuzi wa akiba huku Kamishna wa mchezo akiwa Pius Mashera wa Dodoma.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
http://tff.or.tz/news/633-ligi-kuu-ya-vodacom-tanzania-bara-oktoba-15-n-16
MAANDALIZI SERENGETI BOYS MPYA YAANZA
Tanzania imeanza kuandaa kikosi kipya cha timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys kitakachoshindana kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka hiyo.
Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF), limeiteua Tanzania kuandaa fainali hizo mwaka 2019 hivyo sasa TFF imeanza kuandaa vijana wake.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni