KIKOSI cha Mbeya fc kinatarajia kushuka kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya hapo kesho (Ijumaa) kucheza mchezo mwingine muhimu wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya wageni Stand United kutoka mkoani Shinyanga kikiwa bila nyota wake kadhaa wa safu ya ulinzi.
K wa mujibu wa Ofisa habari, Dismas Ten, maandalizi kuelekea mchezo huo yamekamiliki na City itashuka dimbani ikiendelea kuwakosa nyota wake wawili wa safu ya ulinzi, Haruna Shamte na Sankhani Mkandawile ambao walimua kwenye mchezo wa ugenini dhidi ya JKT Ruvu uliochezwa Mlandizi mkoani Pwani na City kufungwa bao 2-0.
“Kwenye kikosi tunaendelea kuwakosa Haruna na Sankhani, hii ni kwa sababu bado wanauguza majeraha lakini taaraiafa njema ni kuwa mlinzi Rajab Zahir amerejea kikosini kuongeza nguvu baaada ya kushindwa kumaliza dakika 90 za chezo dhidi ya Mwadui kufutia maumivu ya kifungo cha mguu, madaktari wamethibitisha kuwa yuko safi na tayari kwa mchezo wa kesho”, alisema.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni