Mfalme wa Thailand, Bhumibol
Adulyadej, ambaye ni mfalme aliyekaa madaraka kwa muda mrefu,
amefariki dunia baada ya kuwa mfalme kwa muda wa miaka 70.
Mfalme Adulyadej , 88, alikuwa
anaheshimika mno katika nchi hiyo iliyokumbwa na migogoro ya kisiasa
pamoja na mapinduzi ya mara kwa mara.
Mfalme Adulyadej amekuwa katika hali
mbaya ya kiafya katika siku za hivi karibuni na ameonekana mara
chache mbele ya umma.
Mfalme huyo amekufa wakati nchi ya
Thailand ikiendelea kuwa chini ya uongozi wa kijeshi kufuatia
mapinduzi ya mwaka 2014.
Wananchi wakilia kuomboleza kifo cha Mfalme wao Bhumibol Adulyadej
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni