Mke wa rais wa Nigeria Muhammadu
Buhari amemuonya mumewe kuwa anaweza asimuunge mkono kuwania urais
katika uchaguzi mkuu ujao asipofanya mabadiliko katika serikali yake.
Akiongea na shirika la habari la
BBC, Aisha Buhari amesema rais hawajui karibu maafisa wake wote
waandamizi aliowateuwa.
Amesema kunauwezekano serikali ya
Nigeria imetekwa, na kuongeza kuwa kuna watu wachache wanaofanya
uteuzi wa maofisa kwa mamlaka ya rais.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni