.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 14 Oktoba 2016

WAMALAWI WAULIZANA YUPO WAPI RAIS WAO PETER MUTHARIKA

Wananchi wa Malawi wameanzisha kampeni ya kuuliza kama kuna mtu yeyote anayejali kujua alipo rais wao Peter Mutharika.

Rais Mutharika ambaye amekuwa rais wa taifa hilo tangu Mei 2014, alisafiri kwenda kwenye Mkutano Mkuu wa 71 wa Umoja wa Mataifa Jijini New York.

Mkutano huo uliisha Septemba 26 na karibu wakuu wote wa nchi waliohudhuria mkutano huo wamerudi kwenye mataifa yao lakini Mutharika hajarudi.

Hali hiyo imewafanya Wamalawi kuja na hashtag ya #BringbackMutharika, huku wakiikosoa serikali kwa kuficha ukweli kuhusu afya ya Mutharika.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni