Mume wa mwanamuziki wa Marekani,
Mary J. Blige, anashinikiza alipwe fedha ya kujikimu dola 130,000
kila mwezi na mkewe ili aendelee kushi maisha ya kifahari, baada ya
mkewe kuomba talaka.
Mume huyo Martin 'Kendu' Issacs, 49,
anaamini mkewe nyota wa R&B Blige anapaswa kumlipia gharama za
mazoezi, mpishi wake binafsi na posho ya dola 1,000 kwa ajili ya
kununulia mavazi.
Mary J. Blige, 45, amefungua maombi
ya kutalikiana na mumewe Issacs mwezi Julai mwaka huu, kutokana na
sababu ambazo amesema haziwezikupatiwa upatanishi, baada ya miaka 13
ya ndoa.
Mary J Blige akiwa na mumewe Martin 'Kendu' Issacs
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni