Mwanamuziki maarufu wa Jazz nchini
Kenya, ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa kwenye Tusker Project Fame,
Achieng Abura amefariki dunia jana katika hospitali ya Taifa ya
Kenyatta (KNH).
Abura alikuwa amelazwa kwenye wodi
ya binafsi katika hospitali hiyo tangu Oktoba 13, akipatiwa matibabu
ya ugonjwa ambao haujaelezwa.
Mapema mwezi huu mwanamuziki huyo
alitumia mitandao ya jamii, kueleza kuwa hali yake ya kiafya sio
nzuri na madaktari walimshauri aongeze uzito na kisha apunguze
kupitia mazoezi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni