Kiungo Paul Pogba amefunga mara
mbili wakati Manchester United ikipata ushindi mrahisi wa magoli 4-1
dhidi ya Fenerbahce na kukwea hadi nafasi ya pili katika kundi A,
katika mchezo wa Ligi ya Uropa.
Huku ikimrejesha dimbani, Wayne
Rooney, Manchester United haikuwa na madhara sana hadi pale
Fenerbahce ilipotoa penati mbili za kizembe.
Pogba alifunga goli la kwanza baada
ya Simon Kjaer kumchezea rafu Juan Mata na baadaye Anthony Martial
kufunga penati ya pili baada ya kusukumwa na Sener Ozbayrakli.
Pogba aliyeweka rekodi ya uhamisho
alifunga la tatu kwa shuti zuri la mpira wa kuzungusha kutoka umbali
ya yadi 20, na kisha Jesse Lingard kufunga la nne katika umbali kama
huo.
Paul Pogba akiachia shuti lililozaa goli la tatu la Manchester United
Mchezaji wa zamani wa Manchester United Robin van Persie akifunga goli pekee la Fenerbahce
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni