.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 19 Oktoba 2016

NAIBU WAZIRI ABAINI MADUDU HIFADHI YA KIJERESHI

Na Shushu Joel, BUSEGA.

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mwandisi Ramo Makani ameibua madudu makubwa ya ukweukaji mkubwa wa usimamizi wa hifadhi ya kijereshi iliyoko wilaya ya Busega Mkoani Simiyu mara baada ya kufanya ziara ya kutatua kero za mipaka baina ya wafugaji na wahifadhi.

Akizungumza na wananchi wa kata ya mkula mara baada ya kutembelea hifadhi hiyo yenye mgogoro wa muda mrefu kati ya wahifadhi na wafugaji Makani aliweza kubaini mambo mengi ambayo ni kinyume na sheria za uhifadhi lakini yanafanywa na wasimamizi wa hifadhi hiyo na huku meneja akiwa amekaa bila kuchukua hatua sitahiki.

Madudu yaliyobainiwa na Naibu Waziri huyo wa Maliasili na utalii ni kuingizwa kwa makundi ya mifugo katika hifadhi hiyo na huku ni kinyume na taratibu za kisheria na cha kusikitisha zaidi meneja wa hifadhi hiyo ya kijereshi anakana kutokuwepo kwa mifugo hiyo na huku wafugaji baadhi wakikili kuwepo kwa mifugo yao huko ndani ya hifadhi umbali wa kilomita 10 ndani.

Mwandisi Makani amesononeshwa na majibu hayo ya meneja huyo kwa kukataa na kusema kuwa mifugo hiyo ipo Serengeti na si katika hifadhi ya kijereshi kama wanavyodai wafugaji hao.

Akizungumza mbele ya naibu waziri mmoja wa wafugaji ambae Lukoni Kashilimu alisema kuwa yeye tu binafsi amepeleka huko mbungu mifugo 500 na inaishi huko lakini hii inatokana na ukosekanaji wa maeneo ya kulisha mifugo yetu na pia si mimi tu bali tuko wengi ambao tunamifugo huko katika hifadhi.


Aliongeza kuwa mara nyingi huwa tunaelewana nao na kuwapatia kitu kidogo ili wasikusumbue katika hili alisema mfugaji huyo mbele ya naibu waziri huyo.

Aidha alisema kuwa huko mbunganu kuna mifugo kwa zaidi ya 4000 wakichungwa huko kwa lengo la upatikanaji wa malisho mazuri kwa mifugo yetu, tunakuomba waziri uweze kutusaidia tupate maeneo ya malisho kwa mifugo yetu ili tuweze kuondokana na hadha ya kusumbuana na watu wa hifadhi na hata kupeleka ndani ya hifadhi kutakoma kabisa alisema Kashilimu.

Kwa upande wake meneja wa hifadhi hiyo ya kijereshi Nashoni Macokecha alipihojiwa na Naibu Waziri huyo juu ya mifugo kulishwa katika hifadhi hiyo ya kijereshi alidai kuwa mifudo hiyo ipo mbele ya hifadhi ya kijereshi ingawa huwa inapita katika hifadhi ya kijereshi na kuingia Serengeti.

mara nyingi tunafanya dolia kwa ajili ya kufuguza mifugo inayoingia ndani ya hifadhi lakini kwa hili meneja alikaa kuwa katika hifadhi hakuna mifugo iliyoingia kauli ambayo ilikwa ni tofauti na wafugaji wenyewe ambao walisema mbele ya Waziri kuwa hata kama wakimpeleka sasa hivi ndani ya hifadhi hiyo watamuonyesha makundi mengi ya mifugo yao ambayo ipo huko kwa muda mwingi.

                                            >>>>>>>>MWISHO>>>>>>>

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni