Magoli ya kipindi cha kwanza ya
Pierre-Emerick Aubameyang na Julian Weigl yameipatia Borussia
Dortmund ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Sporting Lisbon katika mchezo
wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kundi F.
Bruno Cesar alifungia timu hiyo ya
Ureno kwa mkwaju wa mpira wa adhabu kati kati ya kipindi cha pili,
lakini Borussia walipambana kiume kuulinda ushindi wao huo
unaowafanya wawe na pointi saba.
Pierre-Emerick Aubameyang akifunga goli la kwanza
Pierre-Emerick Aubameyang akiruka sarakasi kushangilia goli lake
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni