Mchezaji Gareth Bale amefunga goli
lake la kwanza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu
2014, wakati mabingwa watetezi Real Madrid wakiichakaza Legia Warsaw
kwa magoli 5-1.
Bale alifunga goli hilo mara tu
baada ya wageni kupiga shuti lililogonga mwamba wa goli Real Madrid
kupitia kwa Vadis Odjidja-Ofoe, kisha baadaye shuti la Marcelo
lilimgonga Tomasz Jodlowiec, na Miroslav Radovic kurudisha moja
kupitia mkwaju wa penati.
Shuti la Marco Asensio la yadi 18,
baada ya mapumziko liliongeza goli la tatu na karamu hiyo ya magoli
ilihitimishwa kwa magoli ya Lucas Vazquez na Alvaro Morata katika
mchezo ambao Cristiano Ronaldo hakuweza kuzifumania nyavu.
Alvaro Morata akiifungia Real Madrid goli la tano
Timu ya Leicester City imebakiza
kupata ushindi mmoja tu kutinga hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa
Ulaya baada ya jana kuifunga Copenhagen kwa goli 1-0 katika dimba la
King Power ikiwa ni ushindi wake wa tatu katika kundi lao.
Riyad Mahrez aliugonga mpira
uliopigwa, Islam Slimani, na kuutumbukiza wavuni katika dakika tano
tu kabla ya mapumziko, na kuifanya timu hiyo kusahau kwa muda
kuvurunda kwao katika ligi kuu ya Uingereza.
Riyad Mahrez akifunga goli pekee katika mchezo huo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni