Lionel Messi amefunga penati katika
dakika za majeruhi na kuisaidia Barcelona kutoka nyuma dhidi ya
Valencia na kuibuka na ushindi wa magoli 3-2 wakiwa ugenini na
kuongoza ligi ya La Liga.
Katika mchezo huo Messi aliipatia
Barcelona goli la kuongoza lililozua utata, baada ya Luis Suarez
aliyekuwa ameotea kuuruka mpira wa chini aliokuwa ameupiga na kujaa
wavuni.
Valencia walipambana na kupachika
magoli mawili kupitia goli la jitihada binafsi la Munir el Haddadi na
Rodrigo kuongeza la pili, lakini Suarez alisawazisha na Messi kufunga
la tatu.
Lionel Messi akiachia shuti la mkwaju wa penati ulioipatia ushindi Barcelona
Wachezaji wa Barcelona Neymar na Suarez wakiwa chini baada ya kupigwa na chupa na mashabiki wa Valencia wakati wakishangilia goli la ushindi



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni