Timu ya Leicester City imefikisha
rekodi ya kutokufungwa nyumbani kufikia michezo 20 baada ya kuibuka
na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Crystal Palace.
Katika mchezo huo Ahmed Musa
aliifungia Leicester goli la kwanza, huku Shinji Okazaki na
Christian Fuchs wakifunga katika kipindi cha pili na kuihakikishia
ushindi.
Yohan Cabaye aliifungia Crystal
Palace goli pekee, huku pia Palace ikilichachafya mno goli la
Leicester katika dakika tano za mwisho.
Ahmed Musa akiwa amejipinda na kuachia shuti lililozaa goli la kwanza
Kipa Mfaransa Mandanda akiwa miguu juu baada ya Okazaki kufunga goli



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni