Timu ya Arsenal imelazimika kutoka
sare tasa na Middlesbrough ikiwa katika dimba lake la nyumbani la
Emirates.
Baada ya kuisambaratisha Ludogorets
Razgrad kwa magoli 6-0 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, Arsenal
ilijikuta ikikabilina na upinzani mkali hii leo licha ya kumiliki mno
mpira.
Middlesbrough inayonolewa na Aitor
Karanka iliendelea kuonyesha upinzani mkali na kuifanya iambulie
pointi moja, dhidi ya Arsenal iliyokuwa imeshinda michezo sita
mfululizo.
Kipa wa Arsenal Petr Cech alikuwa na kazi ya kuokoa michomo hatari ya Middlesbrough
Alexis Sanchez alishindwa kuzuia hisia zake za kuchanganyikiwa baada ya kukosa nafasi ya kufunga



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni