Rais Jacob Zuma amewapongeza
mabingwa wapya wa Soka Afrika timu ya Mamelodi Sundowns ambao
wameshinda Ligi ya Mabingwa CAF.
Rais Zuma pia amewashukuru mashabiki
wa soka na waafrika kusini wote kwa kuiunga mkono timu hiyo na hatua
hiyo imezaa matunda si kwa Sundowns bali kwa taifa zima.
Sundowns wameshinda ubingwa huo
licha ya kufungwa goli 1-0 na Zamalek ya Misri hapo jana usiku.
Sundowns ambao hutambulika kama
Brazil ya Afrika, wameibuka na ushindi huo baada ya mchezo wa awali
kuifunga Zamalek magoli 3-0, na kufanya matokeo ya jumla kuwa magoli
kuwa 3-1.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni