Rais wa Philippine Rodrigo Duterte
amesema kuwa amemuahidi Mungu kuwa atajaribu kuachana na tabia yake
ya kuwa na mdomo mchafu unaomfanya kutoa lugha chafu kwa viongozi
wenzake.
Rais Duterte ambaye ni maarufu kwa
kutoa lugha chafu kwa viongozi wenzake, ametoa kauli hiyo wakati
akiwasili katika mji wa nyumbani kwao wa Davao baada ya kufanya ziara
ya Japan, na kusema Mungu amemtaka kuachana na tabia ya lugha chafu
alipokuwa kwenye ndege.
“Nikiwa angani nilisikia sauti
ikiniambia kuwa acha tabia ya kutoa lugha za matusi ama ndege
itaanguka, na ndipo nilipomuahidi Mungu kuwa ataacha kabisa
kutukana,” alisema rais Duterte.
Duterte aliwahi kumuita rais Barack
Obama mtoto wa kahaba, na kuuita Umoja wa Ulaya kuwa ni umoja wa
kinafiki, pia alitishia kujitoa Umoja wa Mataifa kwa kumfananisha na
Hitler, baada ya kusema angejisikia faraja kuwauwa wafanyabiashara wa
dawa za kulevya milioni tatu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni