Timu ya Real Madrid imeishushia
kipigo cha paka mwizi timu ndogo ya daraja la tatu ya Cultural
Leonesa kwa kuichakaza kwa magoli 7-1 katika mchezo wa kombe la Copa
del Rey.
Katika mchezo huo ambao Madrid
waliwapumzisha Cristiano Ronaldo, Gareth Bale na Karim Benzema,
walipata goli la kwanza baada ya mchezaji wa zamani wa West Brom beki
Gianni Zuiverloon, kujifunga
Magoli mengine ya Real Madrid
yalifungwa na Marco Asensio na Alvaro Morata waliofunga magoli mawili
na Nacho na Mariano walifunga moja kila mmoja.
Gianni Zuiverloon akiwa amempoteza mahesabu kipa wake na kujifunga
Marco Asensio akifunga goli la pili la Real Madrid
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni