Kiwango cha Samir Nasri kimeanza
kumkuna kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps, lakini mchezaji huyo
aliyekataliwa na Manchester City amesema hana mpango wa kubadili
uamuzi wake wa kutoichezea timu ya taifa.
Nasri amesema kuwa hatoichezea tena
timu ya taifa ya Ufaransa hata kama baba yake mzazi atakuwa ndio
kocha wa timu hiyo, na kuongeza kuwa ameshasema mara 100 kuwa yeye ni
mtu anayesimamia kauli zake.
Samir Nasri na kocha Deschamps
wanajulikana kwa kuwa na mahusiano yenye mikwaruzano na kiungo huyo
amekuwa akionekana kuhitajika na timu yake ya taifa tangu atangaze
kujitoa mwezi Agosti.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni