Timu ya Barcelona imepoteza nafasi
ya kukwea kileleni mwa msimamo wa ligi Kuu ya Hispania ya La Liga
baada ya kuduwazwa kwa magoli 4-3 na Celta Vigo katika dimba la
Balaidos.
Iago Aspas alikuwa chachu ya magoli
3-0 katika kipindi cha kwanza, kwa kumtengenezea Pione Sisto goli la
kwanza, kufunga la pili na kulazimisha goli la kujifunga la Jeremy
Mathieu.
Barcelona walipambana na kurejesha
goli kupitia kwa mpira wa kichwa wa Gerard Pique, na penati ya
Neymar, huku kosa la kijinga la Marc-Andre ter Stegen kuwafanya Celta
kufunga goli la nne. Pique alifunga kwa kichwa goli la tatu la
Barcelona.
Mchezaji wa zamani wa Liverpool Iago Aspas akifunga goli la pili la Celta Vigo
Mchezaji nyota wa Brazil na Barcelona Neymar alifunga goli kwa mkwaju wa penati
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni