Italia imepambana na kuambulia sare
ya goli 1-1 katika mchezo wa kuwania kufuzu kutinga michuano ya kombe
la dunia 2018 dhidi ya Hispania kupitia penati ya dakika za mwisho ya
Daniele de Rossi.
Katika mchezo huo uliochezwa nchini
Italia Hispania iliutawala mchezo kwa asilimia 72.4, katika kipindi
cha kwanza lakini ilishindwa kufumania nyavu.
Hispania ilipata goli lake katika
dakika ya 55 baada ya kipa mkongwe Gianluigi Buffon kushindwa kuokoa
mpira na kumpa fursa Vitolo ya kuutumbukiza mpira wavuni.
Kipa Buffon akifanya kosa ambalo lilimfanya Vitolo kupachika goli
Mchezaji De Rossi akigugumia maumivu baada ya kugongwa na mguu wa Diego Costa
Daniele de Rossi akipiga penati iliyoisawazishia goli Italia na kutoa sare




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni