Kocha Gareth Southgate
amepata ushindi wake wa kwanza akiiongoza timu ya taifa ya Uingereza
baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya timu ya taifa dogo
la Malta.
Katika mchezo huo wa kuwania kufuzu
kutinga michuano ya kombe la dunia 2018 Daniel Sturridge na Dele Alli
walifumania nyavu, na kuifanya Uingereza kuongoza kundi F kwa pointi
6.
Katika mchezo huo kapteni Wayne
Rooney ameendelea kutoonyesha kiwango kizuri na kupelekea kuzomewa na
mashabiki wa Uingereza, licha ya kutetewa mno na kocha Gareth
Southgate.
Daniel Sturridge akipiga mpira wa kichwa uliojaa wavuni na kuandika goli la kwanza
Dele Alli akidokoa mpira kwa mguu na kufunga goli la pili la Uingereza
Jesse Lingard akizuiliwa na kipa wa Malta asifunge goli katika mchezo wake wa kwanza akiwa na timu ya taifa




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni