.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 28 Oktoba 2016

UJERUMANI WAIPIGA JEKI SAUTI ZA BUSARA 2017

Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Ndg Simai Mohammed Said akitiliana saini ya Makubaliano ya kusaidia Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar na Balozi wa Ujerumani Tanzania Balozi Egon Kochanke, Ujerumani imekubali kuchangia €5000 sawa na shilingi za Kitanzania milioni 12,hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Kitalii ya Park Hyyat Shangani Zanzibar leo. Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar hufanyika kila mwaka katika mwezi wa Febuary na kuhudhuriwa na Wageni mbalimbali wanaotembelea Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said, akibadilishana mkataba na Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Balozi Egon Kochanke, baada kumaliza kutiliana saini ya makubaliano ya kuchangia Tamasha hilo kwa mwaka 2017, hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Park Hyyat Shangani Zanzibar, leo mchana. Kwa hisani ya ZanziNews

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni