Wafungwa wapatao 25 wameuliwa katika
mapambano baina ya kambi mbili hasimu kwenye gereza lenye wafungwa
wengi kaskazini mwa Brazil.
Polisi nchini Brazil wamesema
wafungwa saba kati ya waliokufa wamekatwa vichwa vyao na sita
miongoni mwao wamechomwa moto na kufa.
Tukio hilo lililotokea huko Boa
Vista, katika jimbo la Roraima, limetokea wakati wa kutembelea
wafungwa katika gereza hilo.
Watu 100 waliokuwa wakitembelea
wafungwa ambao walitekwa na wafungwa wakati wa mapambano hayo
wamekombolewa na vikosi vya kutuliza ghasia.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni