Watu sita wameuwawa kwenye
shambulizi linadaiwa kufanywa na wapiganaji wa kundi la al-Shabaab
katika eneo la makazi la Bulla mjini Mandera nchini Kenya
Tukio hilo limetokea majira ya saa
nane usiku wa kuamkia leo wakati wapangaji wa eneo hilo wakiwa
wamelala, ambapo polisi walifanikiwa kuwaokoa watu 27.
Wavamizi hao walitumia bomo la mkono
kuvunja na kuingia katika makazi hayo na kisha kuwafyatulia risasi
watu waliolala na baadaye kutoroka. Mlipuko mwingine uliathiri paa la
nyumba.
Mmoja wa wapangaji aliyenusuria kwa kupanda juu ya dari baada ya kutokea uvamizi, akiangalia vitu vyake
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni