.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 6 Oktoba 2016

WAKONGWE WAKALI WA KUFUMANIA NYAVU UINGEREZA WAKUTANA


Wachezaji tisa wazamani wa Ligi Kuu ya Uingereza wanaounda klabu ya wachezaji waliofunga magoli 100 na zaidi katika ligi hiyo wamekutana kuhamasisha kuimarisha mpira wa soka Uingereza.

Wachezaji hao tisa ambao ni Ryan Giggs, Dion Dublin, Alan Shearer, Jimmy-Floyd Hasselbaink, Matt Le Tissier, Michael Owen, Les Ferdinand, Emile Heskey na Robin van Persie kwa pamoja wamefunga magoli 1,260.

Wakongwe hao wakali wa kufumania nyavu walikutana kwenye hoteli ya Grosvenor Jijini London kuhudhuria hafla ya 21 ya Malegendari wa soka kusherehekea miaka 25 ya Ligi Kuu ya Uingereza.
Wakongwe hao wakali wa kufumania nyavu wakiwa wamewekewa kifuani idadi ya magoli waliyoyafunga katika Ligi Kuu ya Uingereza

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni