.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 5 Oktoba 2016

WATUMISHI 3 WASIMAMISHWA KAZI ARUSHA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Mashaka Gambo,amewasimamisha kazi watumishi watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za uchaguzi wa mwaka 2015.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Ngorongoro wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa (hayupo pichani),alipokuwa akizungumza nao baada yakufanya ziara katika ofisi za halmashauri hiyo, Wilayani Ngorongoro.
 
Na Mwandishi wetu
 
Watumishi hao ni pamoja na Bi. Hadija Mkumbwa ambae alikuwa msimamizi wa uchaguzi wa mwaka 2015 na kumfuta cheo hicho,bwana Evansi Mwalukasa alikuwa mwekahazina wa halmashauri na bwana Sembeli
Sinayo yeye alikuwa mwanasheria wa halmashauri.

Maamuzi hayo yamefikia baada yakubainika kuna upotevu wa fedha za uchagu takribani Milioni 188 ambazo matumizi yake hayakuwekwa
wazi na pia Milioni 20 zilitumika kwa manunuzi ambayo hayakufuata
taratibu za manunuzi ya serikali.

“Kuanzi sasa nawasimamisha kazi hawa watumishi watatu kwasababu
wameisababishia serikali hasara ya takribani Milioni 128 ambazo zilikuwa fedha za uchaguzi”.

Aidha Muheshimiwa Gambo alisema maamuzi hayo yametokana na taarifa aliyokabidhiwa na kamati aliyoiunda yakuchunguza mapato na matumizi ya fedha za halmashauri hiyo na kubaini upotevu huo wa fedha nyingi
ambazo zingeweza kusaidia shughuli mbalimbali za uchaguzi katika Wilaya hiyo.

Ambapo fedha nyingine zimetumika kwenye manunuzi ambayo hayakufuata taratibu na sheria za manunuzi ya serikali ,hivyo ni kinyume kabisa na taratibu za serikali katika maswala ya manunuzi.

Akisisitiza kwa watumishi wa serikali kufuata taratibu, sheria na kanuni mbalimbali katika kutekeleza majukumu yao ili kuepuka migongano na uvunjifu wa sheria mahala pa kazi nakupelekea kupoteza kazi zao.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni