Andy Murray amemfunga bingwa mara
tano Novak Djokovic na kushinda michuano ya ATP World Tour na
kumaliza mwaka 2016 akiwa mchezaji namba moja duniani.
Wakati mwaka huu ukielekea ukingoni
mchezaji huyo namba moja Murray alishinda fainali hiyo iliyokuwa na
ushindani mkali kwa seti 6-3 6-4 katika dimba la O2 Arena Jijini
London.
Akiongea baada ya ushindi huo Murray
raia wa Scotland, amesema anajisikia vizuri kushinda na kuwa mchezaji
namba moja duniani katika mchezo wa tenesi.
Andy Murray akiwa makini wakati wa mchezo huo
Novak Djokovic akimpongeza kwa kumkumbatia Andy Murray
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni