Goli la kumi la Diego Costa katika
msimu huu limeiwezesha Chelsea kukwea kileleni mwa Ligi Kuu ya
Uingereza na kuizamisha Middlesbrough katika dimba la Riverside kwa
ushindi wa goli 1-0.
Chelsea ambayo hadi sasa haijapoteza
michezo sita mfululizo ilianza kwa kasi katika mchezo huo mgumu na
kufanikiwa kufunga goli pekee katika dakika ya 41.
Kocha wa Chelsea Antonio Conte
amesema anashindwa kuamini ni kwa jinsi gani mabadiliko yanotoendelea
katika timu yake yalivyopelekea kuongoza ligi.
Shuti lililopigwa na Diego Costa kati kati ya msitu wa mabeki likimshinda kipa na kuelekea wavuni
Kipa wa Middlesbrough akifanya kazi ya ziada kuokoa mpira uliopigwa na Pedro
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni