Mahakama moja nchini Marekani
imemtia hatiani baba mmoja kwa kosa la kumuua mtoto wake wa kiume
baada ya kumuacha ndani ya gari juani katika maegesho.
Baba huyo ametiwa hatiani katika
jimbo la Georgia kwa kumuua mtoto wake wa kiume baada ya kumuacha
ndani ya gari lake lililokuwa juani katika maegesho.
Baba huyo Justin Ross Harris, 35,
amekanusha kumuacha kwa makusudi mtoto wake aitwae Cooper, ili afe
kwenye maegesho ya gari ya ofisi yake huko Atlanta.
Harris amesema tukio hilo
lilisababishwa na yeye kusahau kumpitisha mtoto wake na kumuacha
katika kituo cha kulelea watoto wadogo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni