.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 15 Novemba 2016

DC BUSEGA ATANGAZA KIAMA KWA WATUMISHI WALIOKAIDI AGIZO LA WAZIRI MKUU.

MKUU wa wilaya ya Busega mkoani Simiyu, Tano Mwera akisisitiza jambo

                                                                                              Na Shushu Joel,BUSEGA 

MKUU wa wilaya ya Busega mkoani Simiyu, Tano Mwera amewatangazia kiama watumishi wote wilaya humo ambao wameshindwa kutekeleza agizo la Waziri Mkuu, Mh Kassim Majaliwa aliwataka watumishi wa wilaya ya Busega wote kuweza kuhama katika wilaya ya Magu mkoani mwanza ambako walikuwa wanaishi.

Mkuu huyo wa wilaya alitoa agizo hilo alipofanya ziara ya kushitukiza katika ofisi za halmashauri kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa agizo hilo alilolitoa waziri mkuu pindi alipotembelea wilaya hiyo.

“Natoa wiki mbili kuanza leo kila mtumishi anayeishi Magu awe amehamia Busega kwa ajili ya utekelezaji agizo la waziri mkuu ambalo alilitoa kwenu kabla hata sijawa mkuu wa wilaya ya Busega ,sasa nataka utekelezaji wake mara moja la sivyo kama kuna mtu anaona hili agizo kwake ni kero basi akatafute wilaya yake kwa ajili ya utendaji wa kazi huko alisema Tano”

Tano aliwataka wale wote ambao hawajahamia Busega mara moja waweze kufanya hivyo kabla ya wiki mbili la sivyo makubwa yatawakuta, pia amewataka kutofanya kazi kwa mazoea kwani serikali ya JPM si ya kujaribiwa kabisa.

Aliongeza kuwa amesononeshwa na kitendo cha watumishi wengi kutokuwa na nidhamu kwa viongozi wao kwani ni fedhea kubwa kwa watumishi kupinga agizo la waziri mkuu.

Pia amemtaka Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Anderson Ndiginya kuweza kukamilisha kituo cha magari katika mji wa Lamadi ili serikali iweze kujiongezea mapato na kuacha kabisa dhana ya kutegemea serikali kuu huku Busega inao uwezo mkubwa wa kujiendesha na hii ni kutokana na raslimali zilizomo .

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni